WAKILI AZUNGUMZIA KESI YA RAIS WA TFF
Baada ya Rais wa TFF,Jamali Malinzi na makamu wa shirikisho hilo Selestine Mwesigwa kurudishwa rumande hadi july tatu mwaka huu wakishikiliwa kwa makosa 28 ya utakatishaji wa fedha,wakili anaewasimamia viongozi hao ameeleza kwa undani juu ya swala hilo.
Wakili huyo anaetambulika kwa jina la Jerome Msemwa alisema kwamba kwa upande wao wameiomba mahakama isikilize haraka kesi hiyo kwani si utaratibu wa kisheria kuendelea kwa upelelezi wakati kesi iko mahakamani.
Alisema kwamba siku ya jumatatu ya tarehe tatu kesi ya wateja wake itasikilizwa baada ya leo hii kurudishwa rumande,ambapo anaamini siku hiyo kutapatikana ufumbuzi kamili.
Malinzi na Mwesigwa wanaungana na viongozi wa Simba Rais Evans Aveva na makam wake Geofrey Nyange Kaburu ambao nao kwa pamoja wamerudishwa rumande hadi july 13 mwaka huu ambao pia nao wanakabiliwa na shitaka la utakasishaji wa fedha.
Post a Comment