SINGIDA UNITED WATAMBULISHA USAFIRI WAO

Uongozi wa timu ya Singida United ambayo inataraji kushiriki ligi kuu ya Tanzania bara msimu huu leo hii umetangaza rasmi kukamilisha mchakato wa kununua basi jipya la klabu ambalo litatumika kwa shughuli za timu hiyo.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii wakati wa utamburisho wa basi hilo mkurugenzi wa Singida United Festus Sanga alisema kwamba basi hilo aina ya dragon lenye thamani ya shilingi milioni 350 limenunuliwa kwa fedha za klabu ambapo wanaamini hilo ni moja ya jambo kubwa kwa maendeleo ya timu.

Sanga alisema kwamba mbali na swala hilo pia kikosi cha timu hiyo hapo kesho kinataraji kuanza maandalizi kamili kwa ajili ya kujiandaa na msimu wa ligu kuu ya Tanzania bara.

No comments