FRANK LAMPARD AIBWATUKIA ARSENAL, ASEMA HAIWEZI KUMALIZA KATIKA NNE BORA BILA YA MCHILE ALEX SANCHEZ

NA:FREDY REUBEN

Kiungo Wa Zamani Klabu Ya Chelsea Na Timu Ya Taifa Ya Uingereza Frank Lampard Ameibuka Na Kusema Kwamba Arsenal Haiwezi Kumaliza Katika Nne Bora Kunako Michuano Ya Ligi kuu soka Nchini Uingereza Bila Ya Staa Wao Kutoka Taifa la Chile Alex Sanchez.


Lampard Ameyasema Hayo Alipokuwa Akihojiwa Na Kituo Cha Sky Sports Akisisitiza Kuwa Kama Arsenal Inahitaji Kumaliza Katika Nne Bora Basi Ni Lazima Alex Sanchez Awepo Ndani Ya Kikosi Kwani Anauwezo Mkubwa Wa Kuisaidia Arsenal Iweze Kumaliza Katika Nafasi Nzuri Ambayo Itawafanya Arsenal Washiriki Ligi Ya Mabingwa Barani Ulaya (UEFA) Msimu Ujao.


Alex Sanchez Aliwekwa Benchi Na Kocha Mfaransa Arsene Wenger Kwenye Mchezo Dhidi Ya Liverpool Na Kushuhudia Arsenal Wakipoteza Mchezo Huo Kwa Kufungwa Magoli 3_1 Katika Dimba La Anfield Huku Sanchez Akiingia Kipindi Cha Pili Na Kwenda Kuonyesha Uhai Katika Dakika 45 Za Kipindi Cha Pili.


Baada Ya Kuulizwa Ni Kwa Nini Aliamua Kumuweka Nje Mchezaji Huyo Muhimu Ndani Ya Arsenal Ikiwa Tayari Ameshafunga Magoli 20 Ndani Ya Klabu Hiyo Katika Michuano Yote Mpaka Sasa , Wenger Alisema Alihitaji Watu Ambao Wako Vizuri Hasa Katika Kucheza Mipira Ya Juu Ndo Maana Aliamua Kumuweka Nje Sanchez Akiamini Asingeweza Kazi Hiyo Ndo Maana Aliamua Kuwachezesha Dany Welback Na Oliver Giroud.


Alex Sanchez Amebakisha Miezi Michache Tu Kwenye Kandarasi Yake   Lakini Bado Hakuna Mazungumzo Mazuri Kuhusu Kusaini Kandarasi Mpya Ndani Ya Washika Mitutu Wa Jiji La London! Huku Tayari Ameichezea Arsenal Michezo 128 Na Kufunga Magoli 62 Huku akiwa Ametengeneza Magoli 40.

No comments