CHELSEA YAICHAKAZA WEST HAM UNITED, KOCHA ANTONIO CONTE ALIA NA SAFU YAKE YA ULINZI

NA:FREDY REUBEN

Chelsea Imeendelea Kujikita Kileleni Baada Ya Kuweza Kuifunga Klabu Ya West Ham United Magoli 2-1 Katika Uwanja Wa London Stadium Katika Mchezo Ulipigwa Usiku Wa Kuamkia Leo Na Kuifanya Klabu Hiyo Kufikisha Alama 66 Katika Michezo 27 Waliyoshuka Dimbani Mpaka Hivi Sasa.

Chelsea Wamepata Ushindi Muhimu Kwani Michezo Ya London Derby Imekuwa Ikiwasumbua Msimu Huu Baada Ya Kucheza Michezo Mitatu Na Kujikita Wakipoteza Yote, Miwili Kwenye Ligi Kuu Dhidi Ya Arsenal Na Tottenham Lakini Mchezo Mwingine Ilikuwa Kwenye Kombe La Ligi Dhidi Ya West Ham United.

Baada Ya Ushindi Huo Chelsea Wanaongoza Ligi Wakiwa Na Alama 66  Tofauti Ya Alama 10 Dhidi Ya Tottenham Ambae Anashika Nafasi Ya Pili Akiwa Na Alama 56! Huku Anaefuata Ni Manchester City Ambae Tayari Ana Alama 55 Ameachwa Alama 11 Huku Akiwa Na Mchezo Mkononi.

Licha Ya Ushindi Huo Kocha Muitaliano Antonio Conte Amelia Na Safu Ya Ulinzi Ya Klabu Ya Chelsea Baada Ya Kuonekana Kuruhusu Magoli Mengi Katika Kipindi Hiki Cha Karibuni Na Kusema Ni Kitu Hatari Sana Kuelekea Mwishoni Mwa Msimu.

Chelsea Tayari Wameonekana Kuruhusu Magoli Mengi Kipindi Hiki Kwani Mara Ya Mwisho Kutokuruhusu Goli Ilikuwa Ni Kwenye Mchezo Dhidi Ya Hull City Pale Walipoibuka Na Ushindi wa magoli Mawili Kwa Nunge! Lakini Hali Imekuwa Tofauti Kwa Kipindi Hiki Hasa Kuelekea Mwishoni Mwa Msimu.

Chelsea Ambao Kwa Kipindi Cha Nyuma Walicheza Michezo Sita  Mfululizo Bila Kuruhusu Nyavu Zao Kutikiswa Mambo Yamekuwa Tofauti Kwani Katika Michezo Minne Ya Hivi Karibuni Chelsea Tayari Wameruhusu Nyavu Zao Kutikiswa Katika Kila Mchezo  Kitu Ambacho Antonio Conte Amekilalamikia Na Kuona Kuwa Ni Hatari Kwa Upande Wao Hasa Ukiangalia Ushindani Wa Ligi Ulivyo Mpaka Hivi Sasa.

Chelsea wanajiandaa Na Mchezo Wa Kombe La FA Dhidi Ya Mashetani Wekundu Manchester United Mchezo Utakaopigwa Siku Ya J Tatu Katika Dimba La Stamford Bridge! Ikiwa Ni Hatua Ya Robo Fainali Ya Michuano Hiyo!. #Niko_Fair.

No comments