MAWINDO YA RUVU SHOOTING YAANZA LEO

Siku mbili baada ya kurejea  kutoka  jijini Dar Es Salaam kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Simba, kikosi cha Mbeya City Fc  leo kimeanza mazoezi  rasmi kujindaa ‘kutimuana’ na   Ruvu  Shooting  ya Mlandizi mkoani Pwani kwenye  mchezo mwingine wa  ligi hiyo  unaotarajiwa kupigwa siku ya jumamozi ijayo kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.


Afisa habari wa Mbeya City, Dismas Ten amesema, maandalizi kuelekea mchezo huo yanakwenda vizuri lengo likiwa ni kuhakikisha  City  inaibuka na ushindi  na kujiongezea pointi tatu muhimu hasa baada ya kuvuna pointi moja uwanja wa Taifa jumamosi iliyopita kufuatia sare ya 2-2 na vinara wa ligi, Simba Sc


Ten alisema kuwa kwenye mazoezi ya leo,nyota Ayoub Semtawa,Juma Seif Kijiko na Hussein Ahmed walikosekana mazoezini kutokana na kuwa nje ya jiji la Mbeya kwa matatizo ya kifamilia, huku kiungo Mrisharo Ngassa na Zahoro Pazzi waliobaki jijini Dar baada ya mchezo wa Simba wakijumuika na wezao kujiweka fiti kwa ajili ya mchezo huo wa jumamosi.

No comments