YANGA YAREJEA KUTOKA MORO,WAHAMISHIA SILAHA KWA KILUVYA

Msafara wa mabingwa wa tetezi wa ligi kuu Tanzania bara  Yanga SC , umewasili salama jijini Dar es salaam ukitokea Morogoro walipokwenda kucheza na Mtibwa Sugar kwa matokeo ya sare ya 0- 0.

Msafara huo umeelekea moja kwa moja kambini kwa maandalizi ya michezo miwili muhimu itakayofanyika kesho machi 7, 2017 dhidi ya Kiluvya United uwanja wa Taifa na machi 11, klabu bingwa Afrika dhidi ya Zanaco FC.

Timu itaendelea na mazoezi leo jioni kujiandaa na mchezo wa kesho robo fainali kombe la FA dhidi Kiluvya United.

Kocha mkuu wa Yanga SC licha ya ratiba ngumu kuikabili timu yake lakini amesema yupo tayari kupambana na vijana wake ili kuhakikisha klabu inapata matokeo mazuri katika michezo yote miwili.

Kwa mujibu wa uongozi wa klabu hiyo yenye makazi yakemitaa ya Jangwani jijini Dar es salaam umewataka wapenzi , wanachama , mashabiki na wadau wa soka kujitokeza kwa wingi katika michezo yote miwili ili kuipa sapoti timu hiyo .

No comments