NIYONZIMA AREJEA,AWAONDOA HOFU MASHABIKI KUHUSU MECHI YA KESHO NA ZANACO

Kiungo wa klabu ya Yanga Haruna Niyonzima amewataka mashabiki wa mpira wa miguu hapa nchini kuacha kuzungumza maswala ambayo hawana uwakika nayo kwani kufanya hivyo kunapelekea kuleta uchochozi baina ya pande mbili tofauti.


Niyonzima ameyasema hayo baada ya kurejea hapa nchini akitokea Rwanda alipokwenda kwa ruhusa maalumu ya uongozi kushughulikia pasipoti yake.


Amesema kwamba kumekuwa kukizungumzwa taarifa ambazo hazina ukweli juu ya kutokuwepo kwake kambini lakini ukweli ni kuwa alipewa idhini na uongozi kwa siku tatu kwa ajili ya kukamilisha pasipoti yake ambayo ilijaa.


Hata hivyo amedai kuwa anaamini kwenye mchezo wa kesho watafanikiwa kuibuka na ushindi kwani wachezaji wote wapo vizuri na leo hii wamemaliza mazoezi ya mwisho pasipo kuwepo na mchezaji mwenye matatizo makubwa.





No comments