KUWAONA YANGA NA ZANACO NI BUKU TATU TU,ZANACO WAWA KIMYA JUU YA UJIO WAO

Kiingilio cha chini katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 32 bora ya ligi ya mabingwa barani Afrika,kati ya Yanga dhidi ya Zanaco ya Zambia kitakuwa ni shilingi elfu tatu katika mechi hiyo itakayopigwa siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.


Katibu mkuu wa klabu ya Yanga,Charse Boniphace Mkwasa amesema kwamba kiingilio cha juu katika pambano hilo ni shilingi elfu 20 kwa viti vya VIP A.


Mkwasa alisema kwamba uongozi umeamua kuweka kiingilio cha bei nafuu ili kuwapa fursa mashabiki wa Yanga kushuhudia pambano hilo la ligi ya mabingwa ambalo linataraji kuwa na ushindani mkubwa kwa pande zote ingawa wapinzani wao bado wanaweka siri ujio wao hapa nchini.


Aidha alisema kwamba maandalizi kwa upande wao yanaenda vizuri kwa ajili ya mechi hiyo ambapo wachezaji walianza mazoezi mepesi baada ya mechi yao dhidi ya Kiluvya United.

No comments