DOREFA WAIPONGEZA SIMBA

Uongozi wa chama cha soka mkoa wa Dodoma (DOREFA) umeishukuru klabu ya Simba baada ya kuridhia ombi la Chama hicho kucheza mchezo wa kirafiki mkoani humo na timu ya Polisi.


Mwenyekiti wa chama hicho Mlamu Ng'ambi alisema kwamba uongozi wa chama hicho umeridhishwa na hatua hiyo kwani ujio wa Simba mkoani Dodoma utatoa fursa kwa timu za mkoa huo kupata maandalizi mazuri ambayo yatawafanya kurejea katika kiwango kizuri ili mkoa huo upate timu ya ligi kuu.


Ng'ambi alisema kwamba Simba itacheza mechi moja na timu ya Polisi siku ya jumamosi ya tarehe 11 ya mwezi wa tatu mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri.


Aidha alisema kwamba wameamua kuipa mwaliko timu ya Simba kufuatia timu za Azam FC na Yanga kukabiliwa na michuano ya kimataifa.

No comments