MARCO REUS NJE MWEZI MMOJA SASA KUWAKOSA BENFICA

NA:FREDY REUBEN
Kiungo Mshambuliaji Wa Klabu Ya Borusia Dortmund Marco Reus Atakuwa Nje Ya Uwanja Kwa Takribani Wiki Nne Baada Ya Kuumia Nyama Za Paja Kwenye Mchezo Uliopita Walipocheza Na Bayern Leverkusen Na Dortmund Wakiibuka Na Ushindi Mnene Wa Goli 6-2.

Marco Reus Ambae Mpaka Sasa Tayari Ameshafunga Magoli Sita Na Kuchangia Magoli Mengine 7 Katika Michezo 15 Aliyocheza Atakosa Mchezo Wa Marudiano Kwenye Michuano Ya Uefa Champions League Dhidi Ya Benfica Mchezo Utakaopigwa Siku Ya jumatano.

Ukiachana Na Kukosa Mchezo Wa Marudiano Dhidi Ya Benfica Lakini Kiungo Huyo Mchezeshaji Atakosa Baadhi Ya Michezo Ya Bundesliga Ikiwepo Mchezo Kati Ya Ingolstadt Na Hertha Berlin! Huku Ikiwa Ni Michezo Muhimu Kwa Mchezaji Huyo Kuhakikisha Anaisaidia Dortmund Ambayo Mwenendo Wake Sio Mzuri Kwenye Ligi.

Dortmund Walionyesha Kiwango Bora Baada Ya Kuibuka Na Ushindi Mnono Wa Magoli 6-2 Magoli Yaliyofungwa Na Ousmane Dembele Kabla Hajatengeneza Goli Jingine Kwa Mshambuliaji Wa Timu Ya Taifa Ya Gabon Pierre-Emerick Aubameyang Aliefunga Mara Mbili! Huku Magoli Mengine Yakifungwa Na Andre Schurrle, Raphael Guerreiro Na Christian Pulisic Na Kuwafanya Dortmund Wapae Mpaka Nafasi Ya Tatu, Huku Wakiwa Nyuma Kwa Pointi 13 Dhidi Ya Vinara Bayern Munich!#Niko_Fair

No comments