YANGA YAIMALIKA KIUCHUMI,BRANDS ALIPWA MADAI YAKE

Katibu mkuu wa klabu ya Yanga,Charse Boniphace Mkwasa amesema kwamba klabu hiyo haina ukata wa kifedha kama inavyozungumzwa na baadhi ya wadau wa mpira wa miguu hapa nchini.


Mkwasa alisema kwamba kwa kuamini hilo ni kwamba washafanikiwa kulipa deni la kocha Ernestus Brands ambae alikuwa akidai kiasi cha shilingi milioni 25.


Alisema kwamba Yanga ni klabu ambayo inaongoza kuwa na maandalizi bora kwa kipindi hiki na mara nyingi imekuwa ikikaa katika hoteli zenye hadhi kubwa tofauti na timu nyingine.


"Ninachokisema kwamba bado uwezo upo na namna ya kuweza kusafiri na kufanya kazi ya klabu zipo na tuanahakikisha hatuwezi kuacha madeni kwa ajili ya shuguli za mbele na yale madeni sugu tushaanza kuyalipa,Yanga iko vizuri tena sio mchezo sehemu tunayokaa sisi wengine hawawezi keshokutwa tunafunga mkanda tunaenda Zambia sasa wengine wao wanaenda Loliondo"alisema Mkwasa.

No comments