DONALD NGOMA AREJEA MCHEZONI,MBIONI KUWAVAA ZANACO

Kocha msaidizi wa timu ya Yanga,Juma Mwambusi amesema kwamba kikosi cha timu hiyo kinaendelea vizuri maandalizi kwa ajili ya kujiwinda na pambano la klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Zanaco ya Zambia hapo siku ya jumamosi.


Mwambusi alisema kwamba asilimia kubwa ya wachezaji wako vizuri na ana imani watafanikiwa kuibuka na ushindi katika mchezo huo kutoka na hamasa waliyo nayo wachezaji.


Alisema kuwa kuelekea kwenye mchezo huo baadhi ya wachezaji ambao walikuwa majeruhi washaanza mazoezi akiwemo Donald Ngoma pamoja na Amisi Tambwe lakini ushiriki wao katika mechi hiyo ya jumamosi ni mdogo yani 50 kwa 50 lakini lolote linaweza kutokea juu ya wachezaji hao.


No comments