MWAMBUSI ASEMA TFF IMECHANGIA KIKOSI CHAKE KUPATA MATOKEO YA LEO

Kocha msaidizi wa timu ya soka ya Yanga Juma Mwambusi alisema kwamba anaamini kikosi chake kitafanya vizuri katika mchezo wa marudiano dhidi ya Zanaco ya Zambia baada ya leo hii kulazimishwa sale ya kufungana bao 1-1.


 Mwambusi alisema kwamba kushindwa kwao kufanya vizuri leo hii ni kutokana na wachezaji wake kutopata muda wa kupumzika kwa kipindi kilefu kutokana na kucheza mechi za mara kwa mara.


 Aidha amewapongeza wapinzani wao kwa kucheza vizuri hasa kipindi cha pili na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha ambalo kwao limewapa matokeo mazuri.


Katika mechi ya leo winga Saimon Msuva ndie aliyekuwa wa kwanza kuiandikia bao la kuongoza Yanga baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa mchezaji Justine Zulu katika kipindi cha kwanza.


Zanaco walifanikiwa kusawazisha bao hilo katika kipindi cha pili kupitia kwa mchezaji Atram Kwame baada ya kutumia udhaifu wa mabeki wa Yanga ambao walishindwa kujipanga vizuri katika lango lao.


Kwa matokeo hayo Yanga ina kazi kubwa ya kufanya kwenye mchezo wa marejeano kwani wanatakiwa kushindwa kwa ushindi wowote ili wafanikiwe kufuzu katika hatua ya makundi.


No comments