ADI YUSSUF ASEMA TANZANIA IMEJALIWA KUWA NA VIPAJI VYA SOKA

Mtanzania anaecheza soka nchini England Adi Yussuf amesema bado kuna nafasi kubwa kwa watanzania kwenda barani Ulaya na kucheza soka la ushindani kutokana na uwepo wa fursa hiyo.

Adi Yussuf aliwahi kuitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars  chini ya kocha mkuu Charse Boniphace Mkwasa, amesema Tanzania ni nchi kubwa na ina kila sababu ya kutoa wachezaji wengi na wakafanikiwa kupelekea upinzani mkubwa barani Ulaya.

Aidha Adi anaecheza nafasi ya ushambuliaji amekiri kushangazwa na uwezo wa baadhi ya wachezaji wa Tanzania wakati aliporejea nchini kuitikia wito wa kocha Boniface Mkwasa, na mpaka sasa wanaendelea kucheza soka hapa nchini.

Hata hivyo Yussuf amempongeza mchezaji Mbwana Samata ambae anacheza soka la kulipwa nchini Ubelgiji katika klabu ya Genk kwa kusema kwamba mchezaji huyo anatambua kile anachokifanya na anastahili kuigwa na watanzania wote wapenda soka.


No comments