MKWASA RUKSA KUREJEA JANGWANI

Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF limeridhia kocha mkuu wa timu ya Taifa Chars Boniphace Mkwasa kujiunga na klabu ya Yanga endapo kama mwenyewe ataamua kufanya hivyo.
Shirikisho hilo limeyasema hayo kufuatia uvumi uliopo kwamba uongozi wa Yanga uko mbioni kumrejesha Mkwasa kuwa kocha msaidizi wa timu hiyo kufuatia marekebisho yanayoendelea kufanyika kwenye benchi la ufundi la timu hiyo.
Msemaji wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba shirikisho hilo halitakuwa na kikwazo chochote endapo kocha huyo ataamua kufanya hivyo kwani huenda huko aindako akapewa kiasi kikubwa cha fedha ikawa tofauti na kile anacholipwa kwa sasa.
Lucas amesema kwamba ingawa taarifa hizo hazijawa rasmi lkn kama zitakuwepo basi ni vyema Mkwasa akafuata taratibu rasmi za kuvunja mkataba kama alivyofanya wakati anajiunga na timu ya Taifa akitokea klabu hiyo hiyo ya Yanga.

No comments