MWAMBUSI AMZAWADIA HANS USHINDI WA LEO MBELE YA JKT RUVU

Kocha msaidizi wa timu ya soka ya Yanga Juma Mwambusi amesema kwamba ushindi wa hii leo ambao wameupata mbele ya JKT RUVU ya mkoani Pwani wa jumla ya mabao 4-0 ni zawadi kwa aliyewai kocha mkuu wa klabu hiyo Hans ver der Pluijm ambae amejiuzulu nafasi hiyo hapo jana.

Mwambusi amesema kwamba Hans amekuwa ni mtu muhimu kwa upande wake kwani tangu walipoanza kufanya kazi pamoja hawajawi kukwaruzana zaidi ya kuendelea kupeana ushirikiano wa kutosha.

Amesema kwamba yeye ataendelea kumkumbuka kwani alikua mkuu wake na kuondoka kwake ndani ya klabu hiyo ni pengo kubwa lakini licha kuondoka kwake hawataka tamaa kwani watambana hadi dakika za mwisho ili kuiwezesha Yanga inatetea taji lake la ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara.

No comments