MWIGULU AKILI KUMREJESHA HANS VAN DER PLUIJM YANGA

Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba amesema kwamba amechukuwa jukumu la kuongea na kocha mkuu wa klabu ya Yanga Hans van der Pluijm kusalia katika klabu hiyo kwa kuwa hakuona mapungufu yake ya yeye kutokuwepo ndani ya kikosi cha timu hiyo.

Nchemba amesema kwamba mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa pande zote ameona kwamba kuna makosa makubwa ya kiufundi ambayo yamefanyika kwani si jambo jema kufanya marekebisho ya kocha ikiwa timu ipo kwenye mashindano.

"Mimi ni mwanachama hai wa klabu ya Yanga sasa nilivyopata hizi taarifa za kujiuzulu kwa kocha Hans nilishangazwa na maamuzi hayo lakini nimejalibu kuzungumza nae nikamuambia nivyema akapunguza hasira pia nao nimeongea na viongozi nimewaambia haukuwa wakati mzuri wa wao kufanya marekebisho timu ikiwa kwenye mashindano na wote kwa pamoja wakanielewa"alisema Mwigulu.

Katika hatua nyingine Mwigulu amesema kwamba kwa upande wake yeye ana ridhishwa na ufundishaji wa kocha Hans van der Pluijm kwani tangu awepo ndani ya kikosi cha timu hiyo amekuwa na mafanikio makubwa.

No comments