KAGERA SUGAR WAMKINGIA KIFUA MEXME

Uongozi wa timu ya soka ya Kagera Sugar umesema kwamba bado una inami na kocha mkuu wa klabu hiyo Mecky Mexme licha ya baadhi ya mashabiki kuonyesha mabango ya kutokuwa na imani nae ya kuendelea kusalia ndani ya kikosi cha timu hiyo.

Mwenyekiti wa Kagera Sugar Salum Madaki amesema kwamba kwanza anashangazwa na mashabiki wa timu hiyo kudiriki kubeba mabango ambayo hayana msingi kwani kwa hali ilivyo  kocha wao anastahili kupewa sifa kwa jitihada kubwa alizozifanya za kuhakikisha timu bado ipo katika nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi tofauti na msimu uliopita.

Madaki amesema kwamba mashabiki wa timu hiyo wasigetemee kuondoka kwa Mexme ndani ya kikosi hicho kwa wakati huu kwani uongozi bado unaridhishwa na ufundishaji wake licha ya kupoteza michezo miwili mfululizo ikiwemo wa jana dhidi ya Azam ambapo walikubali kufungwa kwa jumla ya mabao 3-2.

No comments