HANS VAN DER PLUIJM AJIUZULU YANGA

Kocha wa timu ya soka ya Yanga Hans van der Pluijm amekabizi barua ya kujiuzulu katika uongozi wa klabu hiyo huku sababu za kujiuzulu kwake zikishindwa kuwekwa wazi kwa wakati huu.

Kwa mujibu wa chanzo cha taarifa hii ni kwamba tayari Hans ameshawakabizi viongozi na wahusika hao tayari wameshaipokea.

Aidha pia taarifa hiyo inadai kuwa kwa sasa kocha msaidizi wa timu hiyo Juma Mwambusi ndie atakaeiongoza Yanga katika mechi zilizosalia hadi hapo kocha mpya atakapoanza majukumu yake.

Takribani wiki hii kumekuwepo na taarifa za ujio wa kocha Mzambia George Lwandamina ambapo kwa sasa yuko jijini Dar es salaam huku taarifa zikieleza kuwa amesaini kandarasi ya miaka miwili.

No comments