TIBOROHA ASHANGAZWA NA MAAMUZI YA UONGOZI WA YANGA
Wakati kukiwa na taarifa kuwa uongozi wa klabu ya Yanga uko mbioni kufanya mabadiliko katika benchi la ufundi ambapo taarifa za awali zinadai kuwa kocha Mzambia George Lwandamina ndie atachukua majukumu ya Hans van dar Plujim,leo hii aliyewai kuwa katibu mkuu wa klabu hiyo Jonas Tiboroha amesema kwamba anashangazwa na maamuzi hayo ambayo huenda yakafanyika ndani ya klabu hiyo kwa kusema kwamba kwa sasa Yanga ilikuwa haina sababu ya kufanya mabadiliko katika benchi la ufundi.
Tiboroha amesema kwamba kwa jijnsi ambavyo anavyoifahamu Yanga kwa muda mrefu kiuhalisia Yanga ilipaswa kufanya marekebisho kidogo kwenye upande wa timu hasa katika sehemu ya ukabaji na mshambuliaji wa kushoto na baadhi ya sehemu katika kikosi hicho.
Kwa upande mwingine Tiboroha amesema kwamba licha ya kuwepo kwa taarifa kuwa uongozi una mpango wa kumpa majukumu Hans kuwa mkurugenzi wa ufundi lakini kwa upande wake haamini kama mabadiliko hayo yatakuwa yanamrizisha kocha huyo.
"Si dhani kama hayo maamuzi kama wamekubaliana na kocha mwenyewe kwa mfano mimi ukiniambia nifanye kazi ambayo naona sistahili kuifanya siwe kukubali hata siku moja nitafanya kazi ambayo naona nastahili kuifanya kwa sasa kazi ya ukuregenzi wa ufundi ni tofauti na kazi ambayo alikuwa anaifanya Hans"alisema Tiboroha.
Post a Comment