MAYANJA AWAPONGEZA MASHABIKI WA SIMBA

 Kocha msaidizi wa timu ya soka ya Simba Jackson Mayanja amewapongeza mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanjani katika uwanja wa Uhuru na kuiwezesha timu kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Totot Africans.
Mayanja amesema kwamba mashabiki wamekuwa na msada mkubwa kwa timu kwani tangu kuanza kwa ligi wameonekana kuiunga mkono timu yao katika mechi mabalimbali za ligi.
Amesema kwamba mbali na kuwapongeza mashabiki pia anawashukuru wachezaji wake kwa kucheza vizuri zaidi katika pambano la leo kwani kila mmoja ameifanyia vyema nafasi aliyoipata.
Aidha amedai kuwa kwa sasa Simba haina mchezaji mwenye namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza kwani yeyeote anaweza kuanza kwenye kikosi hicho ambacho kinaendelea kuongoza ligi kuu ya Tanzania bara

No comments