YANGA YAIPONZA SIMBA KUELEKEA MABADILIKO YA MFUMO

Baraza la michezo la Taifa BMT limeagiza michakato yote inayoendelea ya kubadilisha umiliki wa timu kutoka kwa wanachama kwenda kwenye umiliki wa hisa na ukodishwaji kwa vilabu vyote vya michezo usitishwe mara moja hadi hapo marekebisho ya katiba zao kwa mujibu wa sheria ya Baraza la michezo la taifa na kanuni za msajili.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii katibu mkuu wa BMT,Mohamed Kiganja amesema kwamba baraza linapenda kuona kwamba wahusika wakuu wa jambo hilo hasa klabu za Simba na Yanga wanafuata sheria na taratibu za nchi katika kufikia malengo yao.

Amesema kwamba endapo vilabu hivyo kama vitaendelea na mchakato huo kabla ya taratibu za kurekebisha katiba zao kisheria ni kosa na hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya watakaokiuka maelezo hayo.
"Hivi karibuni imeibuka michakato ya watu wakitaka kubadilisha umiliki wa vilabu vya wanachama na kuvielekeza kwenye utaratibu wa hisa na ukodishwaji,vitendo hivi vimesababisha migogoro mikubwa ambayo inaashiria uvunjifu wa amani ndani ya tasnia ya michezo kwani imefikia hatua watu wanaenda mahakamani mfano mzuri ndani ya klabu ya Yanga"alisema Kiganja.

Ameongeza kuwa makundi ya wapenzi na wanachama wamejikita katika mijadala ambayo hatma yake ni kuzidi kuibomoa jamii badala ya kuijenga na kuimalisha michezo nchini.

No comments