BENEDICKT TINOKO ATIMKIA KWA WAKATA MIWA


Mlinda mlango wa Yanga aliyesajiliwa msimu uliopita kutoka klabu ya Kagera Sugar,Benedickt Tinoko amesema kwamba kwa sasa ameanza rasmi mazoezi katika klabu ya Mtibwa Sugar mara baada uongozi kuafiki kumpeleka kwa mkopo ndani ya klabu hiyo ya wakata miwa wa Manungu Turiani mkoani Morogoro

Tinoko amesema kwamba uongozi wa Yanga umeamua kumpeleka kwa mkopo katika klabu hiyo ksb bado alikua na mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia na amekua hana nafasi ya kucheza ndani ya mabingwa hao wa ligi kuu ya Tanzania bara

Amesema kwamba kwa upande wake ameridhishwa na hatua hiyo kwani inampa chachu ya kurejesha kiwango chake baada ya kushindwa kutamba akiwa na Yanga

Hata hivyo amedai kua anategemea kukumbana na changamoto kubwa kwa makipa wenzake wa Mtibwa Sugar akiwemo Said Mohamed lkn swala hilo halimpi hofu kwani amedhamiria kupambana.

No comments