TFF YAWEKA MSISITIZO JUU YA TAREHE YA MWISHO YA USAJILI WA WACHEZAJI
Shirikisho la
Mpira wa MiguuTanzania (TFF) linapenda kuzikumbusha timu zinazoshiriki Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania Bara kwamba hatutatoa leseni ya mchezaji yeyote ambaye timu
haikuleta mkataba wakati wa maombi ya usajili, hii ni kwa mujibu wa kanuni ya
68 vipengele vya 1, 2, 3 na 8 ya Ligi Kuu ya Tanzania toleo la 2016/2017.
Kila timu
inatakiwa kuleta nakala tatu za mkataba wa mchezaji, ili kamati ya katiba,
sheria na hadhi za wachezaji iweze kupitia na TFF iweze kuidhinisha mikataba
hiyo. Baada ya hapo timu na mchezaji, watakuja kuchukulia mikataba hiyo hapa
TFF. Na kumbuka kanuni ya 68(8) inataka kulipia kiasi cha sh 50,000 kwa kila
mkataba wa mchezaji.
Ni matarajio
yetu kuwa kila klabu itatimiza wajibu wake ili kuondoa migogoro kati ya timu na
mchezaji na mchezaji na timu. Tunategemea kupata ushirikiano.
Kadhalika, kwa
mujibu wa kanuni 67 vipengele vya 1, 2, 3 na 8 ya Ligi Daraja la Kwanza
Tanzania ya StarTimes, Shirikisho la Mpira wa MiguuTanzania (TFF) linakumbusha
kwamba halitatoa leseni ya mchezaji yeyote ambaye timu haikuleta mkataba wakati
wa maombi ya usajili.
Kila timu
inatakiwa kuleta nakala tatu za mkataba wa mchezaji, ili kamati ya katiba,
sheria na hadhi za wachezaji iweze kupitia na TFF iweze kuidhinisha mikataba
hiyo. Baada ya hapo timu na mchezaji mtakuja kuchukulia mikataba hiyo hapa TFF.
Na kumbuka kanuni ya 67(8) inataka kulipia kiasi cha sh 25,000 kwa kila mkataba
wa mchezaji.
Pia katika
hili tunategemea kila timu itatimiza wajibu wake ili kuondoa migogoro kati ya
timu na mchezaji na mchezaji na timu.
Post a Comment