WADHAMINI WA LIGI KUU WAKABIDHI VIFAA KWA TIMU SHIRIKI ZA LIGI KUU YA TANZANIA BARA
Timu ambazo zinashiriki ligi kuu ya Tanzania
bara,zimekabidhiwa vifaa mbalimbali na mdhamini mkuu wa ligi hiyo,vifaa ambavyo
vimekabidhiwa kwa timu shiriki vina thamani ya Zaidi ya shilingi milioni 514
Akiongea katika hafla hiyo ya utoaji vifaa
mtendaji mkuu wa bodi ya ligi,Boniphace Wambura ameishukuru kampuni hiyo,na
kuzitaka klabu shiriki kuheshimu chapa ya mdhamini wakati wote wa mechi za ligi
Amesema kwamba kwa upande wa Bodi ya ligi
maandalizi kwa ujumla yamekamilika ikiwemo waamuzi kupata semina kabla ya
kuanza kwa michuano hiyo ambapo ufunguzi rasmi utafanyika siku ya tarehe 17
ambapo kutakua na mechi kati ya mabingwa watetezi wa kombe hilo,timu ya Yanga
itakapomenyana na makamu bingwa Azam.
Wambura amesema kwamba anaamini msimu huu ligi
itakua bora baada ya kufanya maandalizi mazuri huku akiwasifu waamuzi wa msimu
uliopita kwamba walifuata sheria 17 za soka kwa kua hakuna mwamuzi ambae
amefungiwa hivyo msimu huu watakua bora Zaidi
Hata hivyo amesema kwamba katika ligi ya msimu
huu kuna baadhi ya mechi zitachezwa kwenye uwanja wa Uhuru kwa baadhi ya timu
za Dar es salaam na uwanja mkuu wa Taifa utatumika kwa mechi zenye washabiki
wengi
Post a Comment