MANJI AITISHA MKUTANO MKUU WA WANACHAMA



Uongozi wa klabu ya Yanga ya jijini Dar es salaam umewataka wanachama wa klabu hiyo kuweza kuhudhuria katika mkutano mkuu wa wanachama unaotaraji kufanyika siku ya jumamosi ya tarehe 6 ya mwezi huu kwenye ukumbi wa Daimond Jubliee kuanzia mishale ya saa tatu asubuhi

Kaimu katibu mkuu wa klabu Baraka Deusdedit amesema kwamba mkutano huo wa wanachama utajadili maswala mbalimbali ya klabu na jambo hilo limekuja likiwa na lengo kumaliza mapema swala hilo kabla ya kuanza kwa ligi kuu ya Tanzania bara

Aidha katika hatua nyingine amesema kwamba mbali na mkutano huo pia siku hiyo ya jumamosi kutakua na mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu dhidi ya timu ya Mtibwa Sugar mechi ambayo inataraji kupigwa katika uwanja wa taifa

No comments