WANACHAMA WA YANGA WAMPA TIMU MANJI KWA MIAKA KUMI
Wanachama wa klabu
ya Yanga kwa pamoja wamekubali kumkodisha klabu hiyo Mwenyekiti wao, Yusuf
Manji kwa miaka 10 kuanzia leo ambapo katika kipindi hicho yeye atakua na haki
ya kumiliki timu pamoja na nembo ya klabu
Uamuzi huo umefikiwa katika Mkutano Mkuu wa dharula uliofanyika leo katika ukumbi wa Diamond jubilee, Dar es Salaam ambapo Manji ameomba apewe klabu kwa miaka 10 na katika kipindi hicho atakuwa anachukua asilimia 75 ya mapato ya timu, huku asilimia 25 ikibaki kwa wanachama.
Aidha katika hatua nyingine amesema kwamba swala la
kujenga uwanja wa klabu jambo hilo kwa sasa ni gumu lakini baada ya kupata idhini
ya kumiliki nembo na timu atahakikisha kua atafanya jitihada kubwa kuzungumza
na viongozi wa TFF juu ya maswala ya haki ya matangazo ya televisheni akidai
kua hilo ndio tatizo linalopelekea uongozi kushindwa kujenga uwanja kwa kua
mapato ni madogo
Amesema kwamba vitega uchumi vya klabu yakiwemo majengo
vitaendelea kua mali ya wanachama na hivyo wao watakua na idhini ya kumkodishia
endapo wataridhia kufanya hivyo kwa kipindi chote cha miaka 10
Nae Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la klabu,
Francis Kifukwe amesema kwamba baada ya
wanachama kuridhia mpango huo, wao wanampa pia ridhaa hiyo Manji ya kuiongoza
timu kwa miaka 10
Hata hivyo amedai kua kilichopo sasa
ni baraza hilo la wadhamini kufanya jambo hilo haraka kama alivyohita Manji ili
mchakato huo uanze kutumika
Post a Comment