MAVUGO MBIONI KUSAINI KANDARASI YA MIAKA MIWILI BAADA YA KUTUA MSIMBAZI



Uongozi wa klabu ya Simba umethibitisha kuwepo kwa mchezaji Laudit Mavugo hapa nchini baada ya kuwasili usiku wa kuamkia leo hapa nchini tayari kujiunga na klabu ya Simba

Akiongea na MWANDIKE.BLOGSPORT,mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo Said Tully amesema kwamba,baada ya kuwasili hapa nchini Mavugo anatarajiwa kujiunga na kikosi cha Simba ambapo leo hii kitarejea jijini Dar es salaam baada ya kuwepo mkoani Morogoro kwa takribani wiki mbili kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao

Amesema kwamba uongozi upo mbioni kumpa kandarasi ya miaka miwili kwa ajili ya kuitumikia Simba ingawa mchezji huyo huko nyuma alishasaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo ya mitaa ya Msimbazi.

No comments