MOHAMED DEWJI AWASILISHA BARUA RASMI KWA VIONGOZI WA SIMBA JUU YA OMBI LAKE LA KUTAKA KUNUNUA HISA ZA ASILIMIA 51 KATIKA KLABU YA SIMBA
Mohamed Dewji amesema kwamba leo hii amewasilisha barua katika uongozi wa klabu ya Simba juu ya adhima yake ya kutaka kununua hisa za asilimia 51 kwa kiasi cha shilingi bilioni 20,mara baada ya hapo jana wanachama kuridhia mabadiliko
Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii Dewji amesema kwamba ameshangazwa na kauli za baadhi ya viongozi wa Simba ambazo walizizungumza jana kwenye mkutano mkuu wa wanachama wakidai kua Dewji anajua kuzungumza na vyombo vya habari bila ya kuwasilisha barua rasmi kwa uongozi.
Amesema kwamba kwa upande wake kwa nyakati tofauti amekutana na viongozi wa klabu hiyo akiwemo Raisi Evans Aveva pamoja na makamu wa Raisi Geofrei Nyange Kaburu juu ya swala hilo la kutaka kununua hisa za asilimia 51.
Aidha amedai kua katika barua hiyo ambayo amewasilisha kwa uongozi amechanganua mfumo ambao anataka kuutumia baada ya kukabidhiwa timu kwani lengo lake ni kuona Simba inaingia kwenye ushindani wa soka.
Katika hatua nyingine Dewji amesema kwamba licha ya wanachama wa klabu hiyo kuridhia mfumo wa mabadiliko lkn baadhi ya viongozi akiwemo Raisi wa klabu hiyo ya Simba hawataki mfumo wa mabadiliko
Amedai kwamba anashangaa kuona baadhi ya viongozi wa klabu hawataki mabadiliko wakati idadi kubwa ya wanachama wameridhia mabadilko hayo kwa manufaa ya Simba
Hata hivyo Dewji amesema kwamba yeye kwa sasa ameelekeza nguvu zake kwenye jambo hilo na amewataka viongozi wampe jibu la kukubali mabadiliko kwani nia yake ni kuendelea kuisadia Simba katika maswala mbalimbali na amewahakikishia viongozi kua atakua nao bega kwa bega kusaidia fedha za usajili endapo tu uongozi utaridhia mabadiliko.
Post a Comment