DEWJI AMWAGA FEDHA ZA USAJILI KATIKA KLABU YA SIMBA



Mfanya biashara kijana Mohed Dewji leo hii amewakabidhi viongozi wa Simba hundi ya shilingi milioni 100  ikiwa ni mchango wake kwa ajili ya kuisadia timu hiyo kwenye zoezi la usajili unaotaraji kufungwa tarehe agost sita mwaka huu

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii Dewji amesema kwamba ametoa mchango huo mara baada ya wanachama wa Simba kukuibali mabadiliko na kutimiza ahadi yake ambayo aliitoa mbele ya waandishi wa Habari


Katika hatua nyingine Dewji amesema kwamba anatambua kua mchakato wa mabadiliko utachukua muda mrefu hasa baada mchanganua uliyopo unavyoeneka kufanyika

Amesema kwamba yeye mpango huo alihitaji ufanyike mapema ili apate fursa ya kusajili wachezaji wazuri katika msimu huu lkn kwa sasa jambo hilo ni gumu kwani muda wa usajili unaelekea ukingoni

Hata hivyo amesema kwamba mpango wake bado utaendelea kama alivyopanga na endapo kama viongozi wataridhia mabadiliko anaamini atajenga kikosi bora na chenye ushindani hapo baadae


Nae Raisi wa klabu ya Simba Evans Aveva amesema kwamba kwa niaba ya uongozi unamshukuru Mohamed Dewji kwa mchango wake ambao ameutoa juu ya swala zima la usajili wa wachezaji ndani ya klabu hiyo

Amesema kwamba Simba imekua ikihitaji kiasi cha shilingi milioni 400 kwa ajili ya usajili hivyo kwa mchango wake wa milioni 100 utakua na chachu ya kufanikisha jambo hilo

Hata hivyo Aveva amewataka wanachama wa kalabu ya Simba kuendelea kutoa michango yao kwani  bado kuna upungufu wa fedha za usajili Zaidi ya milioni 300

No comments