TSHISHIMBI ASHINDA TUZO YA MCHEZAJI BORA MWEZI FEBRUARI

Na Said Ally
Kiungo wa timu ya soka ya Yanga Papy Kabamba Tshishimbi ametangazwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Tanzania bara mwezi Februari akiwashinda Emmanuel Okwi kutoka  Simba pamoja na Pius Buswita kutoka Yanga.

Tshishimbi amefanikiwa kuibeba tuzo hiyo baada ya kuisadia vyema timuj yake ya Yanga katika mwezi huo wa Februari akifanikiwa kufunga magoli 3 na kutoa pasi moja ya usaidizi iliyoza bao kwa timu yake.

Kwa kufanikiwa kupata tuzo hiyo Tshishimbi atapata shilingi milioni 1 kutoka kwa wadhamini wa ligi kuu na king'amuzi cha Azam Tv.

No comments