WAMBURA AAMUA KUKATA RUFAA KUPINGA ADHABU YA KAMATI YA MAADILI

Na Said Ally
Aliyekua Makamu wa Rais wa TFF Michael Richard Wambura kupitia kwa wakili wake Emmanuel Muga leo hii wameanza mchakato wa kukata rufaa katika kamati ya Rufaa ya Maadili kupinga adhabu ya kufungiwa Maisha kujihusisha na soka.

Wakili wa Richard Wambura ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba wameaanda Rufaa yenye sababu tano na tayari Wambura ameshalipia kiasi cha shilingi milioni moja kama ada ya ukataji wa rufaa hiyo.

Muga alisema kwamba kuanzia sasa wakati wowote wanataraji kuiwasilisha TFF rufaa hiyo kwa ajili ya kujadiliwa upya hasa baada ya wao kutoridhishwa na maamuzi ya kamati ya maadili.

Alisema kwamba kutokana na sababu tano ambazo wamezibaini kupitia rufaa hiyo anaamini Michael Richard Wambura atashinda swala hilo na kurejea katika soka kama ilivyo awali.

Wambura alifungiwa na kamati ya maadili ya TFF hapo jana baada ya kukutwa na hatia katika makosa matatu ikiwemo kupokea fedha za malipo ambayo hayakuwa halali.

No comments