LIVERPOOL KUMENYANA NA MAN CITY UEFA CHAMPIONS LEAGUE

Timu za England zimepangwa kumenyana zenyewe katika mchuano ya klabu bingwa Ulaya kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo baada ya droo ya michuano hiyo kufanyika leo hii.

Liverpool FC imepangwa kumenyana na Manchester City zote kutoka nchini England katika mchezo huo wa robo fainali ya UEFA.

Mechi kati ya Liverpool ambao wataanza kwa kucheza nyumbani dhidi ya Man City imekuwa gumzo kwa sasa hasa kutokana na timu hizo kutoka nchi moja pamoja na viwango vya timu hizo katika ushindani wa ligi kwenye EPL.

Juventus ya nchini Italy ambayo inaongoza ligi ya nchi hiyo kwa pointi 74 kwa mara nyingine wamepangwa kucheza na Real Madrid ya nchini Hispania iliyo katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na alama 57.

Ikumbukwe kwamba mwaka jana Juventus ilimenyana na Madridi kwenye mechi ya fainali ya michuano hiyo ambapo Real Madrid ilifanikiwa kubeba taji katika fainali hiyo.

Hii inaweza kuwa nafasi kwa Juventus kuweza kulipa kisasi cha kufungwa na mabingwa hao watetezi wa klabu bingwa Ulaya.

Vinara wa Hisapania timu ya Barcelona wao wamepangwa kumenya na AS Roma,mechi ambayo inaonekana ni nyepesi kwa Barcelona kuchomoza na ushindi hasa kutoka na kiwango cha sasa cha Roma kutokua cha kutisha zaidi.

Wababe wa Manchester United timu ya Sevila itakuwa na kibarua kigumu mbele ya Bayern Munchen katika mtanange huo wa robo fainali ambapo Sevila itaanzia nyumbani kuwaalika wababe hao wa Ujerumani.

Sevila ilifanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali baada ya kuiondosha Manchester United katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya vilabu barani Ulaya.

Mechi zote hizo zimepangwa kuchezwa kati ya 3 hadi 11 Aprili mwaka huu.




No comments