KAULI YA YANGA BAADA YA CHIRWA KUTAJWA KUJIUNGA NA DIFAA EL JADID

Na Said Ally
Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kwamba hautakuwa na kikwazo chochote kwa mchezaji Obrey Chirwa endapo mchezaji huyo ataamua kuondoka katika klabu hiyo.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili ndani ya klabu ya Yanga,Hussein Nyika ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kua kwa Sasa wanatambua kua Chirwa bado ni mchezaji wao hadi kufikia Sasa lakini kama ataamua kuondoka klabu haitakua na kikwazo.

Nyika ameyasema hayo kufuatia taarifa ambazo zinaendelea kuelezwa katika baadhi ya mitandao kuwa mchezaji huyo amesaini kandarasi ya awali kwa ajili ya kujiunga na klabu ya Difaa El Jadidi ya nchini Morocco.

Aidha Nyika amesema kwamba kwa Sasa uongozi umeelekeza nguvu zake katika michuano ya kimataifa na ushiriki wa ligi kuu ya Tanzania bara hivyo maswala ya usajili watayaanza baada ya kukamilika kwa ligi mwezi wa tano mwaka huu.

Chirwa kwa Sasa amebakiza miezi miwili kumalizia mkataba wake na hadi hivi Sasa klabu haijampa kandarasi mpya.


No comments