MICHEZO YA ROBO FAINALI YA FA KUCHEZWA MWISHONI MWA MWEZI MARCH

Robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho (Azam Sport Fedaration Cup) inatarajiwa kuchezwa mwishoni mwa mwezi March katika viwanja vinne tofauti hapa nchini.

Ijumaa March 30,2018 kutakua na mchezo mmoja katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga,ambapo wenyeji Stand United watawakaribisha Njombe Mji saa 10:00 jioni.

March 31,2018 kutakua na michezo miwili,Tanzania Prisons watakuwa wenyeji wa JKT Tanzania mchezo utakaopigwa saa 8:00 mchana kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya,huku saa 2:00 usiku Azam FC watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi jijini Dar es salaam.

Jumapili Aprili Mosi,2018 kutakua na mchezo mmoja ambapo Singida United watakuwa wenyeji wa Yanga katika uwanja wa  Namfua mjini Singida,mchezo utakaoanza saa 10:00 jioni.

No comments