NGORONGORO HEROES KUCHEZA MECHI MBILI ZA KIRAFIKI

Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Morocco na Msumbiji kabla ya kuwavaa DR Congo katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za mataifa Afrika kwa vija (AFCON U20).

Ngorongoro Heroes itacheza na timu ya Taifa ya vijana ya Morocco jumamosi March 17, mwaka huu na pia itacheza mechi nyingine  dhidi ya timu ya Taifa ya vijana Msumbiji jumatano March 21,2018 michezo yote ikichezwa kwenye katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON U20,Ngorongoro Heroes itacheza dhidi ya DR Congo March 31 katika uwanja wa Taifa na mchezo wa marudiano utafanyika baada ya wiki mbili jijini Kinshansa Congo DR.

Kikosi hicho cha Ngorongoro Heroes kimeingia kambini katika Hotel ya ndege Beach iliyopo Mbweni ambapo inajiandaa na michezo hiyo miwili ya kirafiki na mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za vijana Afrika wenye umri chini ya miaka 20.

No comments