WAMBURA AFUNGIWA MAISHA KUTOJIHUSISHA NA SOKA

Aliyekuwa makamu wa Rais wa TFF,Michael Richard Wambura amefungiwa kifungo cha maisha cha kutojihusisha na masuala ya soka maisha yake yote baada ya kamati ya Maadili ya TFF inayoongozwa na Hamidu Mbwezeleni kumkuta na hatia ya makosa matatu tofauti ikiwemo kupokea fedha za malipo ambayo hayakuwa halali.

Maswala ambayo yamejadiliwa na kamati ya maadili hapo jana kuhusu swala la Wambura ni pamoja na;
1.Kupokea/Kuchukuwa fedha za Shirikisho (TFF) za malipo ambayo hayakuwa halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(1) cha kanui za Maadili za TFF Toleo la 2013

2.Kughushi barua ya kueleza alipwe malipo ya Kampuni ya JEKC SYSTEM LIMITED huku akijua malipo hayo sio halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013
3.Kufanya Vitendo vinavyoshusha hadhi ya Shirikisho ikiwa ni kinyume na Ibara ya 50(1) ya Katiba ya TFF (Kama ilivyorekebishwa 2015)

No comments