MOHAMED DEWJ ASHINDA NAFASI YA KUWA MWEKEZAJI SIMBA

Na Said Ally
Mfanya biashara Mohamed Dewj MO ametangazwa rasmi kushinda tenda ya kuwekeza ndani ya klabu ya Simba SC kwa mfumo wa Hisa baada ya kutangazwa na jaji Thomas Mihayo katika mkutano uliofanyika leo hii.

Dewji ameshinda tenda hiyo baada ya kuweka dau la shilingi bilioni 20 kwa ajili ya umiliki wa Hisa asilimia 51.

Hata hivyo taarifa ambazo zimepatikana kutoka kwenye mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam zinaeleza makubaliano yaliyofikiwa kwa pande zote ni kwamba MO atapaswa kumiliki hisa za asilimia 49 huku wanachama wakimiliki hisa za asilimia 50%.

No comments