KIKWETE AIFARIJI FAMILIA YA DK.BENDERA

Rais mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete siku ya jana alikuwa miongoni mwa viongozi wa kwanza wa serikali wa nafasi ya juu kwenda msibani maeneo ya Sinza Mori kuifariji familia ya Dk.Joel Nkaya Bendera aliyefariki dunia juzi Desemba 6 mwaka huu.

Mbali ya JK,viongozi na wabunge mbalimbali wakiongozwa na mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi pia waliifariji familia ya marehemu ambaye ana rekodi ya pekee katika soka la nchi hii mbali ya siasa na kazi za serikali.

Joel Nkaya Bendera – Naibu Waziri Mstafu, Mkuu wa Mkoa (mstaafu) wa Manyara, alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Da es salaam.
Familia ya Marehemu Bendera aliyepata kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 1995 hadi 2005 –  Jimbo la Korogwe Mjini, imetangaza kuwa Bendera atapumzishwa kwenye nyumba ya milele Jumapili alasiri katika Kijiji cha Manundu, Korogwe mkoani Tanga.
Joel Nkaya Bendera atakumbukwa kwa mengi ambayo ameyafanya katika soka kutokana na kutovunjwa kwa rekodi yake hadi hivi sasa.
Ndiye kocha msaidizi wa timu ya soka ya Tanzania aliyeongoza Taifa Stars katika kuiondoa Zambia na Tanzania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa Huru ya Tanzania mwaka 1979.
Taifa Stars ilishinda bao 1-0 dhidi ya KK Eleven ya Zambia (sasa Chipolopolo) na kuifanya Tanzania kushiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo mikubwa Afrika kwa upande wa timu za taifa iliyofanyika Nigeria.
Bao lilifungwa na Peter Tino, lakini Taifa Stars haijafuzu tena katika michuano hiyo.
Joel Bendera – ndiye aliyeiongoza Simba kushinda mabao 5-0 dhidi ya Mufulira Wondereres huko Zambia katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1979.
Ikumbukwe kwamba Simba ilifungwa mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza ulifanyika Dar es Salaam.
Joel Bendera – ndiye aliyeiongoza Coastal Union ya Tanga kutwaa ubingwa wa Bara na kucheza michuano ya Afrika Mashariki na Kati na kuifikisha timu hiyo fainali. Wakati akifanya kazi na hayati Zacharia Kinanda.
Joel Bendera – akiwa Naibu Waziri Michezo, chini Waziri George Huruma Mkuchika ndiye aliyeihamaisha Taifa Stars kucheza vema hadi kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN), mwaka 2009.
Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.

No comments