KAULI YA YANGA BAADA YA MOHAMED DEWJ KUSHINDA NAFASI YA UWEKEZAJI SIMBA

Na,Said Ally
Uongozi wa klabu ya Yanga umewapongeza mahasimu wao wa jadi Simba kwa hatua yao kubwa ambayo wameifanya ya mabadiliko ya uendesha wa timu.

Afisa Habari msaidizi wa timu ya Yanga,Godlsten Anderson Chicharito ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba uwamuzi ambao umefanywa na wanachama wa klabu ya Simba na viongozi wao ni jambo jema ambalo linapaswa kuigwa na vilabu vingine.

Chicharito alisema kwamba kitendo hicho ambacho wamekifanya Simba kina tija kubwa hasa katika ukuaji wa soka katika nchi ya Tanzania.

Alisema kwamba kwa kuona umuhimu wa jambo hilo anaamini na wao hawako nyuma kuelekea katika mchakato huo kwa siku za usoni kwani mpira wa miguu kwa sasa unahitaji mabadiliko makubwa ili kuendana na baadhi ya vilabu vikubwa.

No comments