WADAU WA SOKA WAMVAA KOCHA WA KILIMANJARO STARS

Na Said Ally
Wadau mbalimbali wa soka hapa nchini wametoa lawama zao kwa kocha Ammy Ninje baada ya timu ya Kilimanjaro Stars kukubali kupokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Zanzibar Heroes.

Wadau hao kwa nyakati tofauti wametoa lawama hizo wakisema kwamba kocha Ammy Ninje ambae ndie kocha wa Kilimanjaro Stars hana uwezo wa kufundisha timu  hiyo kwani ameshindwa kukipanga vyema kikosi chake katika mchezo wa leo wa michuano ya Challenge inayoendelea kufanyika nchini Kenya.

Mmoja wao alisema kwamba tangu mchezo wa kwanza wa Kilimanjaro Stars waliocheza na Libya kikosi hicho kimeshindwa kuonyesha mchezo mzuri licha ya kupata sale.

Kilimanjaro Stars kwa sasa imejikusanyia alama moja baada ya kushuka dimbani mara mbili katika michuano hiyo ya kombe la Challenge inayofanyika nchini Kenya.


No comments