LIONEL MESSI AIBUA MAZITO, ATANGAZA KUIKACHA ARGENTINA

NA "FREDY REUBEN"
Nyota wa klabu ya Fc Barcelona na Timu  ya Taifa ya Argentina Lionel Messi amesema atastaafu kuichezea Timu ya Taifa ya  Argentina endapo yeye na wachezaji wenzake hawatafanikiwa kufanya vizuri na kulifikisha Taifa hilo mbali  Kwenye michuano ya kombe la Dunia inayotarajiwa kufanyika Urusi hapo mwakani!. 

Gwiji wa Barcelona alisema hatoichezea tena Argentina mnamo mwaka 2016 baada ya kufungwa Kwenye Fainali ya Copa America dhidi ya wabishi Chile lakini Gwiji huyo alirudi miezi miwili baadae!. 

"Kama tutafanya vibaya Kwenye michuano hii mikubwa ya kombe la Dunia tunatakiwa tuondoke wote Timu ya Taifa. Itakuwa ni vigumu kwa mtu YEYOTE kubaki!. 

Tayari Javier Mascherano ambae anacheza na Lionel Messi katika klabu ya Barca  ametangaza atastaafu kuichezea Timu ya  Taifa ya   Argentina baada ya michuano hiyo kukamilika hapo mwakani!. 

"Mascherano??????Sitaki nikwambie nini alichoniambia, lakini naelewa kama ataondoka anahitaji kucheza zaidi na zaidi Alisema Messi!. 

"Namuelewa Mascherano, kitu muhimu ni kucheza na kufurahi wewe mwenyewe, na hafikirii kama atapata dakika za kucheza hapa!.

Messi mwenyewe amekuwa hana wakati mzuri ndani ya Barca kwa namna moja ama nyingine kwa hizi Wiki za karibuni kwani katika mechi mbili za Uefa Champions League ameingia kama mbadala(Sub)  kitu ambacho Messi Hakifurahii!. 

" Benchi kwangu Mimi?? Ni vigumu kutokucheza au kuingia kama mbadala aliongeza Lionel Messi!. 

Argentina wapo Kwenye kundi D kuelekea kombe la Dunia huku katika kundi wakiwa wamepangwa na Nigeria, Iceland na Croatia!. #Niko_Fair

No comments