KILIMANJARO STARS KIBARUANI LEO

Timu ya Taifa ya Tanzania Bara leo Jumapili Desemba 3, inaanza kampeni za kutwaa Kombe la Chalenji dhidi ya Libya katika mchezo wa Kundi A utakaofanyika Uwanja wa Machakos, Kenya.

Kwa mujibu wa kocha mkuu wa timu hiyo Ammy Ninje amesema kwamba kikosi chake kipo tayari kwa mapambano ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu.

Mchezo huo utaanza saa 10.00 jioni (1600h) na kwa Watanzania wote wanaweza kushuhudia kupitia Azam Tv ukitangulia mchezo kati ya Kenya na Rwanda utaaoanza saa 8.00 alasiri (1400h).

No comments