AZAM FC KUANZA KUKIPIGA NA AREA C
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imepangwa na Area C United ya Dodoma katika hatua ya 64 bora ya michuano ya Kombe la FA (Azam Sports Federation Cup).
Droo ya michuano hiyo imepangwa hapo jana katika Ofisi za wadhamini Kampuni ya Azam Media, ambapo mechi zote za hatua hiyo zitafanyika kati ya Desemba 20 na 25 mwaka huu.
Wakati Azam FC ikiwa ni mechi yake ya kwanza ya michuano hiyo msimu huu, Area C inayoshiriki Ligi Daraja la Pili Tanzania Bara (SDL) yenyewe imetoka kucheza hatua ya kwanza na kufanikiwa kuitoa Bulyanhulu ya Shinyanga kwa mikwaju ya penalty 4-3 baada ya suluhu ndani ya dakika 90.
Mabingwa hao wa michuano ya Kombe la Mapinduzi na Ngao ya Jamii wanaodhaminiwa na majia safi ya Uhai Drinking Water na Benki ya NMB, inayoongoza kwa sasa nchini, waliishia hatua ya nusu fainali baada ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Simba.
Katika mchezo huo, Azam FC ilicheza pungufu ya mchezaji mmoja kwa takribani dakika 75 za mchezo baada ya kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy, kuonyeshwa kadi nyekundu yenye utata na mwamuzi Metthew Akrama, akidaiwa kumfanyia madhambi ya makusudi aliyekuwa mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu (sasa Yanga).
Azam FC imepanga kufanya vema kwenye michuano hiyo mwaka huu ikiwemo kutwaa taji hilo na kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho mwaka 2018 au Klabu Bingwa Afrika endapo ikifanikiwa kubeba taji la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
Mechi nyingine 64 bora:
+ Burkinafaso vs Lipuli
+ Green Warriors vs Simba SC
+ Yanga SC vs Reha
+ Mbeya City vs Ihefu FC
+ Villa Squad vs Mtibwa Sugar
+ Kagera Sugar vs Makambako
+ Makanyagio vs Mbao FC
+ Ruvu Shooting vs Madini FC
+ Abajalo vs Tanzania Prisons
+ Njombe Mji vs Mji Mkuu
+ Singida United vs Bodaboda FC
+ Mwadui FC vs Pepsi
+ Majimaji vs New Generation
+ Boma FC vs Ndanda FC
+ Stand United vs AFC
+ African Lyon vs Kiluvya United
+ Biashara United vs Mawenzi Market
+ Mvuvumwa vs JKT Ruvu
+ Coastal Union vs Dodoma FC
+ Polisi Dar vs Mgambo JKT
+ Kariakoo vs Transit Camp
+ Shupavu vs Real Mojamoja
+ Mufindi vs Pamba FC
+ JKT Mlale vs KMC
+ Ambassador vs JKT Oljoro
+ Mshikamano vs Polisi Tanzania
+ Rhino vs Alliance
+ Ashanti United vs Friends Rangers
+ Toto African vs Eleven Stars
+ Majimaji Rangers vs Mbeya Kwanza
+ Mirambo vs Buseresere
Post a Comment