ELIAS MAGULI AZIKACHA SIMBA NA YANGA

Na Said Ally
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Simba na Stend United Elias Maguli kwa sasa yuko mbioni kujiunga na klabu ya Palokwane City inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika ya Kusini (PSL)

Maguli alisema kwamba sasa yuko kwenye mazungumzo na klabu hiyo ya Palokwane na mazungumzo hayo yanaenda vizuri ambapo wakati wowote kuanzia sasa huenda akasaini mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo.

Alisema kwamba mkataba wake na klabu yake ya Dhofar FC ya Omani umesalia miezi sita kuisha lakini hilo halitamzuia kusajiliwa na klabu nyingine kwa kuwa awali kulikuwa na makubaliano ya kuvunja mkataba.

Awali kulikuwa na taarifa za mchezaji huyo kusajiliwa na vilabu vya Simba na Yanga lakini kutokana na taarifa hii imevunja sintofahamu juu ya usajili wa mchezaji Elias Maguli ambae kwa sasa yupo katika kikosi cha timu ya Kilimanjaro Stars kinachoshiriki michuano ya Challenge nchini Kenya.

No comments