AMMY NINJE AWATAKA WA TANZANIA KUIPA SAPOTI KILIMANJARO STARS KWENYE MCHEZO DHIDI YA RWANDA, AKIRI KUFANYA MABADILIKO MAKUBWA

 NA FREDY REUBEN
Kocha mkuu wa kikosi cha Kilimanjaro Stars kinachoshiriki michuano ya Cecafa Senior Challenge huko Kenya, michuano ambayo hujumuisha mataifa kutoka nchi za  Africa mashariki na kati Ammy Ninje amewaomba watanzania kutokukata tamaa na kuendelea kuipa sapoti timu yao huku akiamini nafasi ya kusonga mbele bado ipo licha ya kupoteza alama Tano  katika michezo miwili iliyopita. 

Ninje amewataka wa Tanzania kutokuvunjika Moyo na kuendelea kuwa pamoja na timu yao huku akisema atafanya mabadiliko kwenye mchezo unaofuata ambao utakuwa ni mchezo wa tatu dhidi ya Rwanda hapo kesho. 

Tanzania wamejikuta wapo katika wakati mgumu kuendelea kusonga mbele kwenye michuano hiyo ya Cecafa Senior Challenge baada ya kutoka sare kwenye mchezo wa ufunguzi dhidi ya Libya kabla ya kupoteza mbele ya Zanzibar Heroes kwenye mchezo wa pili uliofanyika siku ya Alhamisi. 

"Mashabiki wanatakiwa watuamini. Hatukucheza vibaya dhidi ya Zanzibar, ni kukosa maamuzi sahihi na umakini kwa wachezaji alisema Kocha huyo alieshuhudia wachezaji wake wakikubali kisago cha goli 2-1 mbele ya Zanzibar. 

Lakini licha ya mlima mrefu ambao Kilimanjaro Stars wanatakiwa kuukwea Ninje bado ana amini nafasi ya kusonga mbele bado ipo licha ya kupoteza michezo miwili ya mwanzo. 

"Bado tuna nafasi. Tunahitaji kushinda mechi mbili zilizosalia.Tutakaa na kuwaambia wachezaji kuwa ni lazima tushinde dhidi ya Rwanda. " 

"Nawaza mchezo na Rwanda kwanza baada ya mchezo huo ndio nitaanza kufikiria mchezo dhidi ya Kenya.Itakuwa ni mchezo mgumu lakini tunahitaji kupigana ili tufikie malengo. 

"Nita angalia kama vijana wapo katika hali gani.Lakini nitafanya mabadiliko na kuwapa nafasi wengine ambao hawajapata nafasi"Alisema Kocha huyo. 

Tanzania inashika nafasi ya nne kwenye kundi ikiwa na alama moja pekee. 

Zanzibar wanaongoza kundi hilo wakiwa na alama sita wakifuatiwa na wenyeji Kenya wenye alama nne katika nafasi ya pili wakati Libya wakiwa nafasi ya Tatu na alama mbili kibindoni huku Rwanda wakiwa wanashika mkia kwenye kundi wakiwa hawana alama hata moja.
#Niko_Fair

No comments