AZAM FC WAWEKA BAYANA SWALA LA MUDATHRI YAHAYA

Na,Said Ally
Uongozi wa klabu ya Azam FC,umesema kwamba kwa sasa hawawezi kumrejesha kiungo mahili wa timu ya Singida United,Mudathri Yahaya kwa kuwa bado ana mkataba wa kimaandishi unaomfanya kuendelea kuwepo katika klabu hiyo ya Singida.

Msemaji wa Azam FC,Jafari Idd ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba licha ya kuwa mchezaji huyo alipelekwa kwa mkopo katika klabu ya Singida United lakini hawawezi kumrejesha kundini kwa kipindi hiki kwani kuna makubaliano maalumu wameyafanya kwa pande zote.

Alisema kwamba uongozi wa Azam FC,ulichukua jukumu la kumpeleka kwa mkopo mchezaji huyo katika klabu ya Singida United ili kunusuru kipaji chake kwani awali alikuwa hapati namba ya kudumu katika kikosi cha timu ya Azam FC.

Aidha alisema kwamba,pindi mkataba wake utakapomalizika Azam watakuwa tayari kufanya nae mazungumzo upya ya usajili kama mchezji mwenyewe atahitaji na pia benchi la ufundi la timu hiyo kuonyesha kuwa na mahitaji nae.

Mudathri kwa sasa ni moja ya viungo bora hapa nchini tangu alipotua katika klabu ya Singida United na pia amefanikiwa kuitwa katika timu ya Taifa inayofundishwa na kocha Salum Shabani Mayanga na ameendelea kuwa mchezji tegemeo katika timu hiyo ya Taifa.

No comments