AMMY NINJE AJINASIBU KILIMANJARO STARS KUFANYA VYEMA KWENYE CHALLENGE

Na,Said Ally
Kocha mkuu wa timu ya Kilimanjaro Stars Ammy Ninje amesema kwamba kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya ushiriki wa michuano ya kombe la Challenge itakayofanyika nchini Kenya kuanzia tarehe 3 ya mwezi desemba.

Ninje ameyasema hayo wakati akiwa katika uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere kabla ya kuanza safari ya kwenda Kenya leo hii.

Alisema kwamba kutokana na maandalizi ambayo ambayo wameyafanya na ubora wa kikosi ambacho amekiteua anaamini uwezekano wa kufanya vizuri upo kwa Kilimanjaro Stars.

Kikosi hicho leo hii kimesafiri kwa shirika la ndege la Kenya KQ tayari kwa ajili ya kushiriki michuano hiyo ya CECAFA ambapo Tanzania itaanza kufungua dimba kumenyana na Libya siku ya tarehe tatu ya mwezi Desemba.

No comments