ZANZIBAR HEROES WAENDA KENYA KWA KUUNGA UNGA

Na Sleiman Ussi,Unguja
Timu ya taifa ya soka ya Zanzibar ( Zanzibar heroes ) leo Alhamisi imeondoka na Jumla ya msafara wa watu 34 wakiwemo viongozi pamoja na wachezaji 24 wameondoka saa 3 za asubuhi  kwa Boti hadi Dar es salam kisha watapanda Basi kwenda mpaka Mkoani Tanga ambapo watalazimika kulala hapo.

Asubuhi yake msafara huo utaanza safari nyingine hadi Mombasa na wakifika Mombasa watapanda Treni itakayowapeleka Nairobi kwa ajili ya kushiriki michuano ya Challenge inayotarajiwa kuanza desemba tatu mwaka huu.

Wachezaji 24 waliochaguliwa kuwakilisha kikosi hicho ni :-

WALINDA MLANGO
Ahmed Ali "Salula" (Taifa ya Jang'ombe), Nassor Mrisho (Okapi) na Mohammed Abdulrahman "Wawesha" (JKU).

WALINZI
Abdallah Haji "Ninja" (Yanga), Mohd Othman Mmanga (Polisi), Ibrahimm Mohammed "Sangula" (Jang'ombe Boys), Adeyum Saleh "Machupa" (Kagera Sugar), Haji Mwinyi Ngwali (Yanga), Issa Haidar "Mwalala" (JKU), Abdulla Kheir "Sebo" (Azam) na Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang'ombe).

VIUNGO
Abdul-swamad Kassim (Miembeni City), Abdul Aziz Makame (Taifa ya Jang'ombe),Mudathir Yahya (Singida United), Mohd Issa "Banka" (Mtibwa Sugar), Amour Suleiman "Pwina" (JKU) na Hamad Mshamata (Chuoni).

WASHAMBULIAJI
Suleiman Kassim "Seleembe" (Majimaji), Kassim Suleiman (Prisons),  Feisal Salum (JKU),  Khamis Mussa "Rais" (Jang'ombe boys), Mwalimu Mohd (Jamhuri), Seif Abdallah “Karihe” (Lipuli) na Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto).

Awali wachezaji hao walikuwa 30 na kulazimika kuachwa 6 ambao wengine waliachwa kwasababu ya majeruhi akiwemo Matteo Anton (Yanga), Ali Badru (Taifa ya Jang'ombe), Salum Songoro (KVZ) na Abubakar Ame "Luiz" (Mlandege) huku wengine walioachwa ni Mbarouk Marshed (Super Falcon) na Omar Juma "Zimbwe" (Chipukizi).

No comments