KILIMANJARO STARS YAWASILI SALAMA NCHINI KENYA

Timu ya Taifa ya Tanzania bara "Kilimanjaro Stars"imewasili salama nchini Kenya siku ya jana tayari kwa maandalizi ya kujiwinda na michuano ya kombe la Challenge itakayoanza kutimua vumbi desemba tatu mwaka huu.

Kikosi cha timu hiyo kimefikia kwenye hoteli ya Gelian na leo hii wamefanya mazoezi kwenye uwanja wa Machakos Academy,mazoezi yaliyofanyika asubuhi na jioni.

Kwa mujibu wa taarifa ya kocha mkuu wa timu hiyo Ammy Ninje amesema kwamba anaamini kikosi chake kitafanya vizuri katika ushiriki wa michuano hiyo ya CECAFA.

Kilimanjaro Stars itaanza kufungua dimba kwa kumenyana na timu ya Libya,mchezo utakaopigwa siku ya jumapili ya tarehe tatu ya mwezi huu.

No comments